| Namba: 249901 | Tarehe: 1390/00/00 | Rejea: | print |
QUR-ANI NA AHLULBAIT NDIO MAREJEO YA UMMA |
Qur-ani na Ahulbait ndio kamba ya Mwenyezi Mungu
Qurani ni kamba ya Mwenyezi Mungu kama Asemavyo Mwenyezi Mungu;
“Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote, wala msitengane”.
“Huenda nikaitwa na (Mola wangu) nami nikajibu, nami ninaacha kati yenu vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu. Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kamba iliyonyooshwa kutoka mbinguni hadi ardhini nacho Kizazi changu ni Ahlubait wangu (watu wa karibu wa nyumbani kwangu). Naye Mwingi wa huruma Aliyemjuzi wa yote amenijulisha kwamba havitotengana kamwe mpaka vitakaponijia kwenye hodhi (ya kauthar). Basi angalieni mtakavyo-vitendea baada yangu”.'Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote…”“Ambavyo mkishi kamana navyo hamtapotea kam-we, (navyo ni) Kitaba cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (ambao ni) Ahlubait wangu”. Neno kamba limetumika katika (maana) kuonyesha kuwa kutoshi-kamana nayo kutamfanya mtu kuanguka kwenye upotofu mkubwa na kuangamia.” “Na mnakanushaje, hali nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu, na Mtume wake yuko pamoja na nyiye? Na mwenye kumshika Mwenyezi Mungu sawa sawa basi yeye amekwishaongozwa katika njia iliyonyooka”“Sisi ndio kamba ya Mwenyezi Mungu ambayo Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka Amesema. “Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msiachane”.“Tulikuwa pamoja na Mtume (s.a.w.a) alipokuja bedui mmoja wa kiarabu na kumwambia “Ya Rasulallah, nilikusikia ukisema “Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu”. Basi ni ipi kamba ya Mwenyezi Mungu ambayo tutashikamana nayo? Mtume (s.a.w.w) akaupigisha mkono wake kwenye mkono wa Ali na kusema “Shikamaneni na huyu, yeye adiye kamba ya Mwenyezi Mungu iliyoimara
Na miongoni mwazo ni hadithi aliyoipokea Annumani kwa isnadi yake kutoka kwa Hariiz Ibnu Abdillah kutoka kwa Abu Abdillah Ja’afar Swadiq Ibnu Muhammad (a.s) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu zake (a.s) kutoka kwa Ali (a.s) ya kwamba alisema,
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) aliho tubia kwenye msikito wa Alkhiif – (Nayo ni hotuba mashu-huri katika hijjatul wida’a (hijja yake ya mwisho) – na kusema” …. Tambueni kuwa mimi ninaacha kati yenu vizito viwili, kizito kikubwa na kizito kidogo. Kizito kikibwa ni Quran, na kizito kidogo ni kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu. Navyo (viwili hivi) ni kamba iliyonyooshwa baina yenu na baina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na Mwenye Nguvu. Mkishikamana nayo hamtapotea kamwe. Sehemu moja yake iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na sehemu (nyingine) iko mikononi mwenu”. “Nemeacha kati yenu viwili vizito (kama) makhalifa (wawili) Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (amboa ni) Ahlubait wangu, (hivi viwili) ni kamba mbili zilizonyooshwa toka binguni hadi ardhini, (na) havitatengana mpaka vitakapanijia huko hodhini (mwa kauthar).Kutotengana kwa Qur-ani na kizazi chake kitukufu (s.a.w.w) milele:
Qur-ani na kizazi kitukufu cha Mtume Muhammad (a.s) ni vyenye kuandamana daima kama mapacha wawili na havitotengana kamwe na vitadumu kuwepo. Hadithi nyingi za thaqalain (vizito viwili) zimesema wazi wazi jambo hili. Kwa mfano kauli yake Mtume (s.a.w.w) isemayo,
“Tambueni kuwa viwili hivi havitatengana kamwe hadi vitakaponijia huko hodhini (mwa kauthar)” Na mfano wa kauli yake nyingine,“Na hakika Mjuzi wa yaliyofichika na yaliyodhahiri Amenijulisha ya kwamba havitatengana kamwe”.“Siku moja babu yangu (Mtume) (sawa) alihotubia. Baada ya kumhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu, alisema” Enyi watu, hakika mimi nitaitwa (na Mola wangu) nami nitajibu, nami ninaacha kati yenu viwili vizito, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu, mkishikamana navyo hamtapotea kamwe. Navyo havitatengana kamwe hadi vitakaponijia kwenye hodhi (ya kauthar). Basi jifun-disheni kutoka kwao na wala msiwafundishe kwani wao ni wajuzi zaidi yenu, na kamwe ardhi haitobaki bila wao. Lau kama itabaki bila wao, basi itaangamia pamoja na watu wake
Hili ni jambo linalokubaliana na akili, kwani ardhi kubaki bila Hujja wa Mwenyezi Mungu (ambaye ni Mtume (s.a.w.w) au Imamu) ni kinyume cha hekima ya Mwenyezi Mungu, hekima ya kutaka kutimiza hoja (yaani itmamul hujja) zake, (kwani Mwenyezi Mungu hawezi kuwaadhibu viumbe vyake kabla ya kuwatumia mwongozo kamili na kuwaonyesha jinsi ya kutekeleza kufwatana na mwongozo huo. wakiwa Mitume na Maimamu ndio waalimu na wafafanuzi wa mwongozo huu, ambapo watu wakiwa watakosa kuufwata watakuwa hawana hoja na dalili ya kujitetea mbele ya Mwenyezi Mungu kwani ameshatimiza na kukamilisha hoja zake kwa kuwapa mwongozo). Kuna hadithi nyingi zinazo elezea jambo hili. Miongoni mwazo ni hadithi zisemazo kuwa:
a) Ahlul bait ni amani kwa watu wa ardhini
Katika kitabu kiitwacho “Fadhailu Ali Ibni Abi Talib” cha Ahmad Ibnu Hambal amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Ali (a.s) ya kwamba alisema,
“Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema, “Nyota ni amani kwa watu wa mbinguni, zitakapoondoka nyota (basi) watu wa mbinguni wataondoka (na kuangamia). Nao Ahlu baiti wangu ni amani kwa watu wa ardhini, watakapoondoka Ahlu baiti wangu (basi) watu wa ardhini wataondoka (na kuangamia)”. “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amesema, “Nyota ni amani kwa watu wa mbinguni, na Ahlubaiti wangu ni amani kwa umma wangu, zitakapoondoka nyota, (basi) watu wa mbinguni wataondoka na wata-kapoondoka Ahlubaiti wangu (basi) watu wa ardhini wataondoka (na kuangamia)”.b) Ukhalifa wa Makhalifa wa Mtume (s.a.w.w) na Mahujja wa Mwenyezi Mungu utaendelea hadi siku ya kiama
Alhamwani amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Abdullah Ibnul Abbas ya kwamba alisema:
“Kwa hakika Makhalifa wangu na Mawasii wangu na Mahujja wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe baada yangu (watakuwa) kumi na wawili wa mwanzo wao ni ndugu yangu na wa mwisho wao ni mwanangu”. Akaulizwa “Ya Rasulallah, na ni nani ndugu yako?” Akasema, “Ali Ibnu Abi Talib” akaulizwa, “Na ninani mwanao?” Akajibu, “Almahdi ambaye ataijaza ardhi kwa usawa na uadilifu baada ya kujazwa kwa ujeuri na dhulma. Naapa kwa yule Aliyeniteuwa kwa haki kuwa mbashiri, lau kama ardhi itakuwa haijabakisha ila siku moja, Mwenyezi Mungu Atairefusha hiyo siku ili Amdhihirishe mwanangu Almahdi. Basi (siku hiyo) Atamshusha Isa Ibnu Maryam (kutoka mbinguni) naye ataswali nyuma yake (Almahdi) na hapo ardhi itanawiri kwa nuru ya Mola wake, na utawala wake (Almahdi) utafika mashariki na magharibi.” “Nilimtembelea Mtume (s.a.w.w) nikampata Husein akiwa (ameketi) mapajani mwake, huku (Mume) (s.a.w.w) anayabusu macho yake na mdomo wake na kumwambia, “wewe ni bwana, mwana wa bwana (seyyid), ndugu wa bwana, na baba wa mabwana. Wewe ni Imamu, mwana wa Imamu, ndugu wa Imamu, na baba wa Maimamu. Wewe ni Hujja mwana wa Hujja ndugu wa Hujja baba ya mahujjah tisa watokanao na kizazi chako, wa tisa wao akiwa ndiye Alqain (Almahdi).” “Nilimsikia Mtume (s.a.w.w) akisema, “Mambo ya watu yataendelea kutangamana madamu watu kumi na wawili wanawatawala”, kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu alitamka neno ambalo sikulipata, basi nilimu-uliza baba yangu “Je, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amesema nini?” akasema “Amesema, “wote watatokana na Qureish”. “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akisema “Dini itaendelea kuwepo hadi siku ya kiama, na wataendelea kuwatawala Makhalifa kumi na wawili wote wanaotokana na Qureish.”Hadith thaqalain inaonyesha kuwa Ahlul bait (a.s) ni maasumu.
Hii hadithi tukufu inaonyesha kuwa Qurani na Ahlul bait ni maasumu kwani imemdhaminia mwenye kuvifwata (hivi viwili) kwamba hatopotea wala kuangamia, bila ya kumwekea sharti lolote. Ni wazi kuwa haingetoa dhamana hii lau kama havingekuwa maasumu.
Kuna hadithi nyingi za thaqalain zilizotamka waziwazi kwa maneno haya, kwa ibara tofauti tofauti.
a) Miongoni mwazo ni,
“Enyi watu hakika mimi ninaacha kati yenu ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (ambacho ni) Ahlubaiti wangu”.
“Ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka, pamoja na kizazi changu Ahlu baiti wangu”. “Huyu Ali yuko pamoja na Qurani, nayo Qurani iko pamoja na Ali, hawatatengana hadi watakaponijia huko hodhini (mwa kauthar)”.“Ewe Allah, ipitishe haki pamoja naye popote alipo”.
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amesema “Hakika mfano wa Ahlubaiti wangu kati yenu ni mfano wa jahazi ya Nuhu, aliyeipanda aliokoka na aliyebaki nyuma (bila kuipanda) alighariki.” “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amesema, “kwa hakika mfano wa Ahlubaiti wangu ni mfano wa mlango wa “hittah” kwa wana wa sraeli, aliyeingia (ndani yake) alisame- hewa (madhambi yake).”Uhusiano wa kizazi chake kitukufu(s.a.w.w) na Mwenyezi Mungu
a) Kauli yake Mtume (s.a.w.a) isemayo:
“Viwili hivi ni kamba iliyonyooshwa toka binguni iliyoko baina yenu na Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka.”b) Na kauli yake (s.a.w.w)
c) Na kuali yake (s.a.w.w)
“Upande mmoja wake (kamba hii) uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na upande mwengine uko mikononi mwenuHakika hivi viwili havitatengana kamwe hadi vita-kaponijia huko hodhini (mwa kauthar)”.e) Na kauli yake (s.a.w.w)
“Mkishikamana navyo hamtapotea kamwe“Huyu Ali yuko pamoja na Qurani, nayo Qurani iko pamoja na Ali (Hivi viwili) havite-ngani.”(Basi msiwatangulie msije mkahiliki na wala msibaki nyuma yao msije mkaangamia”.“Hakika” hivi viwili ni makhalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).“Mja anapoteuliwa na Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu na Aliyetukuka ili kuyasimamia mambo ya waja wake, humpanulia kifua chake kwa ajili yake (kazi hii) na huweka moyoni mwake chemchemu za hekima, na humfunulia elimu sawa sawa (kwa njia ya) ilhamu (kiasi cha kuwa) hashindwi katika kutoa jawabu, na wala hapatwi na shaka na jawabu iliyo ya haki”.Wajibu wa kuwafuata Ahlulbait ni sawa na wajibu wa kukifuato Kitabu cha Mwenyezi Mungu
Lililo la wajibu ni kuwafuata Ahlulbait kama ilivyowajibu kukifuata Kitabu Kitukufu (Quran). Hili ndilo linalo kusudiwa na hadithuth thaqalain. Basi haitoshi kuwaheshimu tu na kudhihirisha mapenzi na mahaba bila ya kuwafwata. Dalili ya haya tusemayo, ni kule kufanywa Ahlul bait kuwa kizito cha pili pamoja na Quran, pamoja na kauli yake Mtume (s.a.w.w).
“Basi msiwatangulie na wala msibaki nyuma yao” na kauli yake“Mkishikama navyo hamtapotea”.“Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alishaamuru kuwa ifuatwe Qurani (pamoja) na Aali Muhammad (kizazi chake) pale aliposema katika hotuba yake ya mwisho (kabla ya kufarikiana na dunia)” Hakika mimi ninaacha kati yenu viwili vizito, kizito kikubwa na kizito kidogo. Ama kikubwa ni Kitabu cha Mola wangu na ama kidogo ni kizazi changu (ambacho ni) Ahlubaiti wanguKutopingana kwa hadith thaqalain na ile iliyopokewa katika Majmauz Zawaid
Jua ya kwamba hadithi iliyopokelewa kwenye kitabu cha Majmauz Zawaid kutoka kwa Abu Huraira ya kwamba Mtume (s.a.w.w) alisema;
Vile vile baadhi ya hadithi zinazosisitiza kushi-kamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume (s.a.w.w) hazipingani na hadithi mutawatir zinazosisitiza juu ya kushikamana na Kitabu na kizazi, kwani sunna ya hakika na iliyosahihi haipatikani ila tu kutokana na kizazi kiongofu. Kwa hivyo, hakuna mgongano wala mpingano kati ya hadithi hizo ikiwa hadithi hii itakuwa imethibiti kuwa imetoka kwa Mtume (s.a.w.w) Ama hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ya kwamba alisema,
“Hakika mimi ninaacha kati yenu vitu viwili, (ambavyo) baada yavyo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na nasaba yangu. Na havita-tengana kamwe hadi vitakaponijia Kwenye hodhi (ya kauthar)”.Kwanza
Kwa hivyo basi hadithi hii dhaifu haina nguvu na uwezo wa kuipinga hadithuth thaqalain iliyomutawatir na isiyo kuwa na shaka ndani yake kuwa imetoka kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w).
Pili: Pamoja na kuwa hadithi hiyo ni dhaifu pia inapingana na ijmai (makubaliano na maafikiano ya maulama wote) na akili pia, kama anavyosema Allama Mir Husein “Hakika hadithun nujum (hadithi ya nyota) inaonyesha kuwa maswahaba wote wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) walikuwa wema, ambapo, kufuatana na ijmai sivyo hivyo kamwe. Vile vile inaonyesha kuwa wote ni wenye kuungoza umma (katika njia iliyonyooka) ambapo sivyo pia, kwani kikundi kikubwa kati yao kiliwapoteza watu wengi. Vile vile inaonyesha kuwa maswahaba wote wanastahiki kufuatwa na umma na hilo pia ni jambo lisiloweza kuwa sahihi kamwe kwani wengi wao walikuwa ni watu wenye kasoro ambazo ziliwafanya wasistahiki hilo”.
Hadi kufikia kusema, “Zimeteremka aya katika Kitabu cha Mweneyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka, zinazoelezea wazi wazi hali za kikundi kikubwa cha maswahaba, na hasa aya zilizoko katika sura ya Anfal Bara-ah, Ahzabi Jum-ah na ya Munafi-quun. Basi je Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) anaweza akawateuwa maswahaba wote wake kuwa viongozi wa umma na hali kama hii?”.
Mpaka kufikia kasema, “zimepokewa hadithi nyingi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) zenye kuwalaumu na kuwashusha daraja baadhi ya maswahaba, utakazozi-pata kwenye Sihahu na Masanid zenye kutegemewa. Miongoni mwazo ni “hadithul haudh.” (Hadithi ya hodhi) “hadithul irtidad” (hadithi ya kuritadi kwa maswahab) na hadithi isemayo “msirudi baada yangu makafiri”, hadithi isemayo kuwa “ushirikina ndani yenu umejificha zaidi ya kutambaa kwa sisimizi”, hadithi isemayo “sijui mtakayoyafanya baada yangu”, hadithi isemayo, “mtaufuata mwenendo wa mayahudi na manaswara”, na “hadithut tanaafus” (Hadithi ya kushindana), hadithi isemayo, “katika maswahaba kuna ambaye hatoniona (huko peponi) nami pia sito-mwona”, hadithi isemayo “katika maswahaba wangu kuna wanafiki”, hadithi isemayo, “wenye kunizulia uwongo wamezidi”, na nyingi nyinginezo ambazo zinawalaumu baadhi ya maswahaba. “Na zipo hadithi katika vitabu vya ndugu zetu masunni zinazoonyesha waziwazi kuwa Mtume (s.a.w.w) alikataza na kuzuia kufuatwa maswahaba kama hao. Katika baadhi yazo, ame sema.
Maulamaa wakubwa wa kisunni wameta-mka wazi wazi kuwa hadithi hii ni dhaifu. Mwandishi wa kitabu cha “Abaqatul Anwar” amewataja baadhi yao katika utangulizi wa kitabu chake. Miongoni mwao (aliowataja) wakiwemo Ahmad Ibnu Hambal, Albazzaz, Addaru Qutni Ibnu Hazm, Albaihaqi, -hata ingawa yeye mwenyewa anainakili hadithi hiina Ibnu Asakir, Ibnul Jauzi, Ibnu Duhya, Abu Hayyan, Adh-dhahabi, Ibnul Haitham, Ibnu Hajar Al-asqalani na wengineo katika wale waliosema waziwazi kuwa hadithi hio sio sahihi au kuwa ni dhaifu au kuwa Mtume (s.a.w.w) alizuliwa (hadithi hii). “Kwa kiasi chochote kile mlichopewa (kili choko) katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu basi yeyote yule hana udhuru wa kutokitenda. Na ikiwa hakipo ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu. basi (kitapatikana) katika Sunna yangu na ikiwa hakikupatikana katika Sunna yangu basi(kitapatikana) katika yale wasemayo maswahaba wangu. Hakika maswahaba wangu ni mfano wa nyota zilizo binguni, yeyote (kati yao) mtakayemfuata, mtaongokaHadi kufikia kusema.
“Hakika mwenye kuwafwata hao ataingia motoni.”Tatu: lau kama tutakubali kuwa hadithi hii ni sahihi, lakini tunapata kuwa haipingani na hadithuth thaqalain kwani inaingia na kuambatana na yale yote yaliyo tajwa kwenye hadithi ya thaqalain, kwa kuwa imewaamuru (waislamu) kutenda, kufuatana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kusema kuwa mwenye kupuuza kutenda hayo hana udhuru (wa kutoa). Kisha ikiwa ufafanuzi kuhusu kitu haupatikani katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi (hadithi), imeamuru kuwa ifuatwe sunna ya Mtume (s.a.w.w.). Na ikiwa sunna haipatikani (hadithi) ikaturejesha kwa maswahaba. Na ni wazi kuwa sunna sahihi na ya hakika wako nayo Ahlul bait wa Mtume (s.a.w.w) na kuwafuata hao ni wajibu wa daraja ya mbele. Basi Ahlul bait wanapo-kuwepo hakuna nafasi ya kuwafuata maswahaba.
Nne: Hakuna awezaye kukanusha tofauti iliyo-kuwepo baina ya maswahaba katika kuzinukuu huku-mu za Mwenyezi Mungu na mambo mengineyo kuto-kana na kutojua kwa wengi wao. Hata wao wenyewe walikiri kuwa hawakuwa na elimu. Hivyo basi itawezekanaje kwa Mtume(s.a.w.w) kuwafanya kuwa marejeo ya umma katika maongozo ya kidini pamoja na kuthibiti ujahili wao na kuhitilafiana baina yao.
Haya, tukiongeza pia vitendo vya haramu walivyo-tenda baadhi yao, kama vile kuuza pombe, kuchukua riba katika biashara, na vinginevyo, vilivyotajwa katika Kitabu cha “Abaqatul Anwar”. Audhubillah!! kutokana na kumnasibishia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) mambo kama hayo, (Mtume) aliye-teuliwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaongoza watu.
Mtume(s.a.w.w) ametukuka na ametakasika kutokana na kunasibishiwa mambo kama hayo. Hii ni kufuatana na hukumu ya akili na hadithi zilizomutawatir, ikiwa miongoni mwazo ni hadithuth thaqalain, ambayo kama ujuavyo, iliubainishia umma njia iliyonyooka isiyo kuwa na upotofu. Basi mwenye kuipuuza hiyo njia kwa madai hayo, kwa hakika atakuwa ameiacha njia iliyonyooka na kujiingiza kwenye upotofu, husuda, chuki na ushindani, hayo yote ni miongo ni mwa mambo ambayo yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w), naye akatilia mkazo kwa kusema,
“Naye Alhanafi amesema (amepokea), “kutatokea fitna baina ya maswahaba wangu, Mwenyezi Mungu atawasamehe kwa yale waliyo yatanguliza. Watu watakao kuja baada yao wakiwafuata Mwenyezi Mungu awatumbukize katika moto wa Jahanam.”“Hakika mimi nitawaulizeni kuhusu vitu viwili, Qurani na kizazi changu”.
Hadith thaqalain inathibitisha kuwa Uimamu ni wa kizazi cheke(s.a.w.w) pekee
Hadithuth thaqalain inaonyesha kuwa kizazi cha Mtume (s.a.w.w) kilipata Uimamu baada tu ya Mtume (s.a.w.w) kuaga dunia bila ya kupita muda na kwa hivyo hilo ndilo linalofaa kufuatwa kama tuonavyo katika hadithi zilizomutawatir zinazoonyesha kuwa Mtume (s.a.w.w) alimfanya Imam Ali (a.s) kuwa wasii khalifa na walii (kiongozi) baada yake.
Na hii ndio sababu Seyyid Murtadha (r.a) katika Kitabu cha Shafii ananukuliwa akisema “Hadithi hii inaonyesha kuwa Amirul Muumini Ali (a.s.) alikuwa ndiye Imamu baada ya Mtume (s.a.w.w) pasipo kupita muda”.
Mwenye kushikamana na Qurani na kizazi chake(s.a.w.w} kitukufu, ndiye muongofu
Mwenye kushikamana na Qurani na kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w) huyo ndiye aliyeongoka kufuatana na kauli ya Mtume (s.a.w.w) aliye mkweli na mwaminifu, katika hadithuth thaqalain iliyomu-tawatir. Na wala haifai kumwita mpotofu au raafidhi (mkataa haki) mwenye kushikamana navyo, kwani Mtume (s.a.w.w) hakosei katika kauli yake. Kuna hadithi nyingi zionyeshazo kuwa mashia, wafuasi wa Ahlul bait (a.s) ndio watakaofuzu siku ya kiama. Basi (ndugu yangu) usighafilike.
Kwa kumalizia ninamuomba Mwenyezi Mungu awajaalie ndugu zetu waislamu kutafakari katika hadithuth thaqalain, iliyomutawatir na inayokubaliwa na maulama wa madhehebu yote ya kiislamu.
Kwani hadithi hiyo ni nuru ambayo Mtukufu Mtume(s.a.w.w) aliwaangazia waislamu ili wasije wa-kapotea wala kufarikiana, baada ya kuondoka kwake.
Ewe Allah, tujaalie sisi na waislamu wote ulimwe-nguni, kushikamana na Kitabu Kitukufu na Kizazi chake Kitoharifu, Amina ya rabbal alamina.
.” Hiyo hadithi haikuba-liki kwa sababa nyingi. Nazo ni kama zifuatazo: Hadithi hii haipingani kamwe na hadithi zilizomutawatir (nyingi) zinazoonyesha kuwa Mtume (s.a.w.w) aliacha Kitabu na kizazi chake, kizazi chake (Al-itra) ni Jamaa wa karibu wa Mtume, kwa hivyo basi kutumia neno nasaba (katika hadithi ya Abu Huraira) kunachukuliwa kuwa kusudio lake ni wale wa karibu. Na kusudio hili la wale jamaa wa karibu linajulikana kuto kana na kanuni iitwayo “Munasabatul hukmi wal maudhu”, kusudio lake sio kuwafuata jamaa wote wa karibu ambako kutamfanya mtu aongoke, bali kusudio lake ni jamaa maalum ambao ni maasum, kama zionyeshavyo hadithi nyingi ambazo tulizoashiria na kuzitaja baadhi yake hapo awali..
Na ni wazi kuwa kushikamana na kizazi ni kutenda kufuatana na kauli zao na maagizo na makatazo yao na kuufuata mwenenda wao Mtukufu.
Hii ndio sababu tunamuona Taftazani ananukuliwa akisema baada ya kuitaja hadithi hii, “Je huoni kuwa (Mtume(s.a.w.w) aliwataja pamoja na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka (kwa kusema) kuwa kushikamana navyo viwili kunamuokoa mtu kutokana na kupotoka. Kushikamana na kitabu hakumaanishi ila tu kuchukua katika elimu na mwongozo wake na (hiyo ndiyo maana ya kushikamana na) kizazi vile vile!!
Imepokewa kuwa Ibnu Hajar amesema kuwa, Mtume (s.a.w.w) aliwahimiza watu kuwafuata, kushi-kamana nao na kuchukua elimu kutoka kwao.
Na hii inamaana kuwa maamrisho na makatazo yatokanayo na kizazi kitukufu ni lazima yafuatwe kama ilivyo wajibu kuyafuata maamrisho na makatazo ya Qurani tukufu.
Ikidaiwa kuwa maamrisho na makatazo yao ni hayo hayo maamrisho na makatazo ya Qurani tukufu, sisi tutajibu kwa kusema, maamrisho na makatazo yao ni mapana zaidi, kwani huenda wakati mwengine yakatoka kwa unwani kuwa wao ni Mawalii(viongozi) juu ya mambo yote ya umma, nayo nikufuatana na hadithi iliyotuamrisha sisi kufuata maamrisho yao na kuacha makatazo yao bila ya kupunguza wala kuongeza chochote, na hiyo ndiyo maana ya “wilaya mutlaqa” yaani uongozi usio kuwa na mipaka.
Mwandishi wa Abaqatul Anwar amefaidisha na kufanya wema aliposema: “Hakika hadithi (hii) inamaaniisha kuwa ni wajibu kuwafuata Ahlul bait katika maneno yao, vitendo, hukumu na itikadi zote. Na ni dhahiri kuwa cheo hiki na cha namna hii hakiwezi kupatikana ila tu kwa yule ambaye amefikia daraja ya Uimamu na Uongozi mkuu (wa cheo cha juu kabisa) baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).
Naye Seyyid Sharafu Din amesema “Zimepokewa hadithi nyingi zilizo mutawatiri na sahihi zinazoonye-sha na kuelezea wajibu wa kukifuata kizazi cha Mtume (s.a.w.w) .
Na hasa hadithi zilizopokelewa kwa njia za upokezi za kizazi kitoharifu, (yaani kwanye vitabi vya hadithi vya kishia).
Kwa hivyo basi kuifasiri hadithi hiyo eti kuwa inauusia umma kukipenda na kukiheshimu kizazi hicho kitoharifu na wala sio (kwamba kuna uwajibu wa) kuwafuata, kunapingana na yaliyomo kwenye hadithi hiyo kama vile kukitaja kwenye hukumu moja na Quran na kukiweka sawa nayo na kuwazuia watu kukitangulia au kubaki nyuma ya kizazi hicho, kuam-risha kushikamana nacho, na kuchukua kutokana nacho hakumpi mtu nafasi ya kuifasiri hadithi hii kama walivyoifasiri. Hii nipamoja na dalili nyingi-nezo, zinazomzuia mtu kuifasiri vivyo.
Kwa hivyo basi sababu hasa ya kusema kuwa Quran na kizazi kitoharifu, vimejaaliwa kuwa Maima-mu katika kuwaongoza watu imefahamika. Hili ni jambo lililowazi katika hadithuth thaqalain, kama alivyosema Imam Ja’afar Swadiq (a.s.),
,Hizi pamoja na nyinginezo nyingi ni dalili zionye-shazo wazi ukaribu wa kizazi kitukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, na ya kuwa walikuwa wakiongo-zwa na Mwenyezi Mungu.
Huu uhusiano nao na Mwenyezi Mungu na ukaribifu wao mbele yake ndio uliowafanya kuwa tofauti na watu wengine. Na ndio sababu twasema kuwa Uimamu wao haukuwa sawa na Ukhalifa wa makhalifa wa ndugu zetu masunni, kwa sababu ya tofauti ya kiasili iliyoko baina ya Uimamu huu na Ukhalifa huo.
Uimamu kwetu una asili moja na Utume, bali tofauti iliyoko baina yao ni wahyi uliyomakhsusi kwa Mitume. Ama Mwongozo wa Mwenyezi Mungu wa kighaibu (kwa njia isiyokuwa ya wahyi) ungali unaendelea, nao Maimamu waongofu wamechukua majukumu yote ya Mtume (s.a.w.w) aliyotwikwa na Mwenyezi Mungu.
Hii ni kinyume cha Uimamu (Ukhalifa) kwa ndugu zetu masunni. Kwani wao wanauchukulia kuwa utawala na uongozi wa dhahiri, bila ya kulazimisha umaasumu na uadilifu katika Imamu (Khalifa).
Hata hivyo hadithuth thaqalain imetuthibitishia kuwa Uimamu una maana ile ile iliyotajwa katika kizazi kitukufu cha Mtume(s.a.w.w).Basi wao Maimamu wamechukua vyeo vile vya Mtume (s.a.w.w) kama vile uongozi wa kidini na uongozi wa kisiasa, ila tu tofauti iliyoko baina yao na Mtume (s.a.w.w) ni kwamba wao wanachukua sheria za uislamu kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na wanamfuata yeye (s.a.w.w) katika mambo yote na wanaongozwa kwa nuru yake na ni Makhalifa wake katika umma wake. Basi wanachukua majukumu yake yote ikiwa miongoni mwayo, ni utawala wa hukuma (serikali).
Kwa hivyo basi, maana halisi ya Uimamu kwetu ina tofautiana na maana halisi ya Uimamu kwa ndugu zetu masunni. Hadithi inatusaidia pamoja na dalili za kiakili zinazo kubaliwa na wenye akili wote, kuthibitisha jambo hili, na ndio sababu mashia ithnaasharia wakatofautiana na waislamu wengineo katika kuitakidi kudumu na kuendelea kuwepo uhusiano wa kighaibu na mwongozo wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuendelea kuwepo kizazi kitoharifu cha Mtume (s.a.w.w).
Imamu wetu wa nane, Imam Ali Ridha (a.s) amasema.”
g) Vlie vile kule kuwafananisha na jahazi ya Nuhu (a.s.) au kuwafananisha na nyota, pamoja na kauli yake isemayo.
f) Au kauli yake (s.a.w.w)
”d) Na kauli yake (s.a.w.w)
.”Seyyid Sharafudin (r.a) amesema kwamba, “sababu hasa ya kufananishwa kwa Ahlulbait na mlango wa hitta ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Aliufanya mlango huo kuwa ni dhihirisho mojawapo la unyenyekevu mbele ya utukufu wake na utiifu mbele ya hukumu yake na kwa hivyo, hii ikawa ndio sababu ya kupata maghfira (msamaha), Vile vile (Mwenyezi Mungu) Amejaalia pia utiifu wa umma huu kwa Ahlulbait wa Mtume wake (s.a.w.w) na kuwafwata Maimamu hao kukuwa ni dhihirisho mojawapo la unyenyekevu mbele yake na utiifu mbele ya hukumu. Na kwa hivyo hii ikawa ndio sababu ya kupata maghfira. Hii ndio sababu ya wao kufananishwa na mlango huo.
Hata hivyo baadhi ya maulama wa kisunni wamekiri jambo hili, miongoni mwao akiwa Razi, Ibn Hajar Alhaitami, Aljalalus suyuti, Assanad na wengineo.
Ibnu Abil Hadid amemnukuu Abu Muhammad Ibnu Muttawaih kutoka kwenye kitabu cha “Alkifaya” akisema, “Hakika Ali (a.s) ni maasumu hata ingawa sio kwa isma (umaasumu) ya wajibu, na wala isma sio sharti kwa Imamu lakini dalili za kisheria (Quran na hadithi) zimethibitisha ya kwamba yeye ni maasumu na mwenye yakini, na ya kwamba hili ni jambo linalomhusu yeye pekee, wala maswahaba wengine hawakupewa. Tofauti katika maneno yetu iko wazi tunaposema “Zaid ni maasumu” na tunaposema “Zaid ni maasumu kiwajibu, kwa kuwa yeye ni Imamu na katika masharti ya Imamu ni kwamba awe ni maasu-mu”. Kauli ya kwanza inaambatana na dhehebu letu la (kisunni) na kauli ya pili inaambatana na dhehebu la Imamiya (mashia)”.
Jua ya kwamba, Qur-ani imekuwa maasumu kwa kuwa imetoka kwa Mwenyezi Mungu Ambaye hapa-twi na kosa katika vitendo vyake na wala katika kuiteremsha Qurani, au katika kuwateremshia Mitume (a.s) wahyi wake na katika kuwafikishia watu, kwani lengo la kuwaongoza watu ni kuwafikisha kwenye maslahi yao halisi na ya hakika. Basi, ikiwa Mwenyezi Mungu atafanya kinyume cha hayo atakuwa amefanya kinyume cha hekima yake tukufu.
Vivyo hivyo umaasumu (isma) wa Maimamu ni kwa kuwa elimu yao imetokana na Mtume (s.a.w.w) na Mwenyezi Mungu na kwa hivyo elimu zao haziwezi kupatwa na makosa wala kasoro, kwani wao wame-teuliwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaongoza watu na kuwatakasa, na kama tujuavyo makosa na upotofu hayasaidii katika kulifikia lengo hili tukufu na wala hayanasibiani na hekima ya Mwenyezi Mugu.
Kwa hivyo basi Qurani na kizazi kutukufu cha Mtume (s.a.w.w) ni maasumu, na vyote viwili vimehi-fadhiwa kutokana na makosa, na kuvifwata kunamhi-fadhi mtu katokana na kuangamia. Hii ikiwa ni fadhila ya kipekee, na iliyomakhsusi kwa hivi viwili tu.
f) Na miongoni mwazo ni aliyoipokea Attabarani kutoka kwa Abu Said, aliyesema kwamba,
Hizi ni pamoja na dalili nyinginezo, kama vile ayatut tathir inayoonyesha na kuthibitisha umaasum wa Ahlul bait, pamoja na hadithi mutawatir zinazoon-yesha kuwa hao ni maasumu.
e) Na Miongoni mwazo ni hadithi aliyoipokea Alhaakim kwa isnadi yake kutoka kwa Abu Dhar ya kwamba alisema:
d) Na miongoni mwazo ni dua ya Mtume Mtukufu (s.a.w.a) aliyomsomea Ali (a.s) kwa kusema”
c) Na Miongoni mwazo ni zile zilizotamka wazi wazi,
b) Na Miongoni mwazo ni;
Pamoja na riwaya nyingi nyinginezo.
Na hii ndiyo sababu tunamuona Samhudi ananakiliwa kwenye kitabu cha “Jawahirul Aqdain” kutoka kwenye kitabu cha “Tanbihatuth thaqalain” akisema kuwa “Hii inaonyesha kuwepo kwa watu wanaostahiki kushikamanwa nao, miongoni mwa Ahlul bait na kizazi kitoharifu, katika kila zama wanapokuwepo hadi siku ya kiyama. Na ndio sababu hadithi zikasisitiza katila kushikamana nao, kama zilivyosisitiza kuhusu Quran tukufu. Na hiyo ndiyo sababu, kama tutakavyoelezea baadaye, wakawa ni amani kwa watu wa ardhini, ambapo wa kiondoka nayo ardhi itaondoka”.
Vile vile Ibnu Hajar katika kitabu chake “Assawaiqul Muhriqa”, na katika hadithi zinazosisitiza katika kushikamana na Ahlul bait, kuna ishara kuwa wata-endelea kushikamanwa nao hadi siku ya kiyama, kama Qurani tukufu ilivyo, na ndiyo sababu wakawa ni amani kwa watu wa ardhini”.
Alhamwini amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Nafii ya kwamba alisema”,
Muslim katika kitabu chake “Sahihu Muslim” amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Jabir Ibnu Samura ya kwamba alisema”.
Almuwaffaq Ibnu Ahmad (mmoja katika maulama wakubwa wa kisunni) amenukuu hadithi kutoka kwa Salman Almuhammadi ya kwamba alisema”.
Na katika “Aamal” cha Sheikh Attusi kwa Isnadi yake kutoka kwa Ibnu Abbas, ya kwamba alisema,
”.Hizi zilikuwa habari za ghaibu na bishara kuhusu kubaki kwa Qurani na kizazi kitukufu hadi siku ya kiyama. Bishara ya kuonyesha kuwa Qurani tukufu na kizazi, vitadumu kuwepo na hakuna wakati ambao havitakuwepo. Kama vile Qurani ni muujiza wa milele, vile vile kizazi cha Mtume (s.a.w.w) ni muujiza wa milele na kamwe hakitakosekana ardhini (hiki kizazi).
Kuna hadithi nyingi pia zilizotamka waziwazi jambo hili, mfano wake ni ile iliyopokewa na Sheikh Suleiman Alhanafi Alqanduzi kwa isnadi yake kutoka kwa Imam Hasan (a.s) ya kwamba alisema,
Kwa hivyo basi, la wajibu kufanya katika kuleta umoja na kuondosha utengano na ufarikiano, ni kushikamana na vizito viwili na kuzuia utengano kabisa, kwani hivi ndivyo vinavyoleta umoja, kama ilivyo kuwa katika zama za Mtume (s.a.w.w) umoja ulipatikana kwa kushikamana na Mtume wake (s.a.w.w). Yatupasa basi, sisi waislamu, kuamka kutoka usingizini na kushikamana na sababu muhimu na ya asili ya umoja wetu. Ndipo tutakuwa tumepata umoja wa kweli tulioamrishwa kuwa nao katika aya tukufu, na umoja huu utakuwa umeondoa umoja wa juu juu, hata ingawa ni umoja unaofaa, unaostahiki kuwepo.
Kisha kuiita Qurani na kizazi kwa jina la kamba ya Mwenyezi Mungu kunaonyesha wazi uhusiano mkubwa vilivyonao na Mwenyezi Mungu, kwa hivyo mwenye kushikamana navyo atakuwa kwa hakika ameshikamana na Mwenyezi Mungu. Na kunaonyesha pia kuwa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu ndio njia ya pekee ya kujihifadhi kutokana na upotovu.
Na miongono mwazo ni hadithi aliyoitaja Ibnu Abil Hadid, ya kwamba Mtume (s.a.w.a) alisema,
”.Vile vile mwandishi wa Kitabul Manaqib ame-pokea kutoka kwa Said Ibnu Jubair (R.a) kutoka kwa Ibnul Abbas (R.a) ya kwamba alisema:
Katika aya hizi ni dhahiri kuwa kushikamana na aya za Mwenyezi Mungu na kumfwata Mtume (s.a.w.w) ni sawa na kushikamana na kamba ya Mwe-nyezi Mungu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika aya iliyotangulia, kwamba kushikamana navyo ni kushikama na Mwenyezi Mungu, kwa hivyo basi kama vile Mtume (s.a.w.w) ni mfano wa kamba ya Mwenyezi Mungu, vile vile kizazi chake kitukufu chenye kuchukua cheo chake (baada yake) ni mfano wa kamba ya Mwenyezi Mungu.
Haya pamoja na kuongezea riwaya nyingi zilizoe-lezea wazi wazi jambo hili. Miongoni mwazo ni riwaya iliyopokewa kwenye Abaqatul Anwar kutoka kwa Sheikh Suleiman Al-hanafi Alqanduzi katika tafsiri ya aya “Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote…” alisema kuwa “Ath-tha’alabi amepokea kwa sanadi yake (silsila ya wapokezi) kutoka kwa Aban Ibnu Taghlib kutoka kwa Ja’afar Swadiq (R.a.) ya kwamba alisema.
Dalili nyingine inayo tuthibitishia kuwa neno kamba halikutumiwa makhsusi kwa Qurani, bali lime-wakusanya pia Ahlul bait, ni kuwa, Mtume(s.a.w.w) amekusanywa kwenye maana hii katika aya
Mwandishi amesema, “yaani jizuieni kutokana na kuanguka, kwa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu mkiwa katika hali ya umoja, na (pia) kwa kushikamana na) kile ambacho amekijaalia kuwa ni chenye kuwahifadhi (na kuwazuia) kutokana na kuanguka kwenye upotofu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ameshatu julisha kuwa ni nani wanaoitwa kamba, ambayo mwenye kushikamana nayo hapotei, katika kauli yake kwenye hadithuth thaqalain isemeyo:
Kuna riwaya nying zinazoshuhudia jambo hili. Miongoni mwazo, ni riwaya aliyoipokea Abu Said Alkhidri kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ya kwamba alisema,
Vile vile kamba ya Mwenyezi Mungu inawaku-sanya Ahlulbait (a.s), kwa kuwa wamefanywa kuwa sawa na Quran katika hadithuth thaqalain, na kwa kuwa wameteuliwa na Mwenyezi Mungu kuwaongoza watu. Basi kushikamana nao ni sawa na kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu ambayo inatuzuia na kupotoka na kuangamia.
Katika Tafsiru Alaur Rahman’ baada ya kuitaja aya hii,