Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Mwonekano wa utu wa Imam
Namba: 256681 Tarehe: 1390/00/00Rejea: print

Mwonekano wa utu wa Imam


 Mwonekano wa utu wa Imam

Sifa za ukamilifu zilikusanyika kwa Imam Ali bin Abu Talib. Alikuwa
na sifa nzuri za kusifika, mahsusi za kupendeza, nasaba bora na shara-
fu tukufu, asili takatifu na nafasi yenye kuridhiwa. Sifa ambazo
hakubahatika kuzipata mtu yeyote mwingine, kwani yeye ni jemedari
wa waumini, mbora wa mawasii na khalifa wa kwanza wa Mtume
(s.a.w.w.) kati ya makhalifa waongozao kwa amri ya Mwenyezi
Mungu.

Maelezo ya Mtume  (s.a.w.w.) na Qur’ani tukufu vimeeleza wazi
kuhusu umaasumu wake dhidi ya kila uchafu.  Mtume (s.a.w.w.)
akaapizana na wakristo wa Najran kupitia yeye, mkewe, na wanawe
wawili
.  Pia alimfanya ni kati ya ndugu zake wa karibu ambao
tumewajibishwa  kuwapenda
 huku  mara  kwa  mara  Mtume

(s.a.w.w.) akitueleza wazi kuwa wao ni sawa na Kitabu kitukufu, hivyo huokoka yule atakayevishika viwili hivyo na huangamia yule atakayeviacha.

Imam Ali bin Abu Talib (a.s.) aliishi zama za Mtume (s.a.w.w.) na
utume, kuanzia pale ufunuo ulipoanza kushuka mpaka ulipokatika
kwa kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) huku akiwa na
nafasi ya juu ambayo hutamaniwa. Nayo ni katika kumhami Mtume
(s.a.w.w.) na utume muda wote wa miaka ishirini na tatu, ikiwa ni
jihadi yenye kuendelea na mapambano endelevu ya kuhami Uislamu na tukufu zake. Hivyo misimamo yake, utendaji wake na sifa zake vimejiakisi katika Aya za Kitabu kitukufu na maelezo ya hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Ibnu Abbas amesema: “Ziliteremka Aya mia tatu kuhusu fadhila za Ali (a.s.), hakuna Aya iliyoteremka na ibara ya: “Enyi mlioamini” isipokuwa Ali (a.s.) ndio kiongozi na mlengwa wa mwanzo katika Aya hiyo. Hakika Mwenyezi Mungu amewalaumu wafuasi wa Muhammad katika baadhi ya Aya za Qur’ani lakini hakumtaja Ali (a.s.) isipokuwa kwa heri.”

Kutokana na kukithiri Aya zilizoteremka kuhusu fadhila za Ali (a.s.) baadhi ya wasomi wa zamani wameandika vitabu mahsusi ambavyo vimekusanya  Aya  zilizoteremshwa  kwa  ajili  yake.  Hivyo  hapa tutaashiria baadhi ya Aya ambazo wanahadithi wameeleza wazi kuwa ziliteremshwa kwa ajili yake.

Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa:  “Ali  (a.s.) alikuwa na
dirhamu nne tu huku akiwa hana nyingine, hivyo usiku akatoa sada-
ka  dirhamu  moja,  mchana  dirhamu  moja,  na  dirhamu  nyingine katika hali ya rukuu. Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza mwombaji: “Ni
nani aliyekupa pete hii?” Akajibu: “Ni yule aliye katika hali ya rukuu,
hapo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya isemayo: “Hakika kiongozi
wenu khasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walioamini
ambao  husimamisha  Swala  na  hutoa  Zaka  na  hali  ya  kuwa
wamerukuu.”

Aya ya utakaso imemfanya Ali (a.s.) kuwa kati ya Ahlul-Bayt wa
Mtume (s.a.w.w.) ambao wametakaswa dhidi ya kila uchafu, huku
Aya ya maapizano ikimfanya kuwa nafsi ya Mtume (s.a.w.w.).

Ama Sura Insan imeashiria ukunjufu wa moyo aliyonao Ali (a.s.) na
watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) na jinsi wanavyomwogopa
Mwenyezi  Mungu.  Pia  imebeba  ushahidi  wa  Mwenyezi  Mungu
kuthibitisha kuwa wao ni watu wa peponi. Waandishi wa vitabu
Sahihi sita na wengineo miongoni mwa wanazuoni wa hadithi wame-
tenga milango mahsusi ndani ya vitabu vyao inayoelezea fadhila za
Imam Ali (a.s.) kupitia hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Wanadamu ndani ya historia yao ya muda mrefu hawajamwona mtu
bora  kuliko  Ali (a.s.)  baada  ya  Mtume  wa  Mwenyezi  Mungu

(s.a.w.w.). Wala hakuna mtu ambaye fadhila zake zimeandikwa kama
zilivyoandikwa fadhila za Imam Ali (a.s.). Japokuwa muda wote wa
utawala wa kizazi cha Umayya maadui na wanafiki walimwelekezea
matusi na kashfa juu ya mimbari zao wakiwa na lengo la kumtia

akaitoa sadaka kwa siri na nyingine kwa dhahiri, hapo Mwenyezi
Mungu akateremsha Aya isemayo: “Wale watoao mali zao usiku na
mchana, kwa siri na dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao,
wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.”

Ibnu Abbas amesema: “Ali (a.s.) alitoa sadaka pete yake huku akiwa dosari, lakini hawakupata sehemu yoyote kwake yenye dosari na
aibu.

Kati ya kauli za Umar bin Al-Khatab ni:  “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: ‘Hakuchuma mchumaji mfano wa fadhila za Ali, kwani  yeye  humwongoza  mfuasi  wake  kwenye  uongofu  na humzuwia dhidi ya maangamio.”

Imam Ali (a.s.) aliulizwa: “Kwa nini wewe una Hadithi nyingi kuliko
maswahaba wengine wa Mtume (s.a.w.w.)?” Akajibu: Hakika mimi
nilikuwa nimuulizapo ananijibu, na ninyamazapo hunianza”.

Imepokewa kutoka kwa Ibnu Umar kuwa: Siku Mtume (s.a.w.w.) ali-
pounga undugu kati ya maswahaba zake, Ali alikuja huku macho yake
yakidondoka machozi, hapo Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Ali (a.s.):
“Wewe ni ndugu yangu hapa duniani na kesho Akhera.”

Imepokewa  kutoka  kwa Abu  Layla Al-Ghaffariy  kuwa  alisema:
“Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Baada
yangu itatokea fitina, basi ikitokea hali hiyo shikamaneni na Ali bin
Abu Talib, hakika yeye ndiye wa kwanza kuniamini, na ndiye wa
kwanza atakayenipa mkono siku ya Kiyama, yeye ni mkweli mno, na
yeye ndiye atakayefarakisha kati ya haki na batili ya umma huu, yeye
ndiye jemedari wa waumini na mali ndio jemedali wa wanafiki.”

Makhalifa wote wamekiri kuwa Ali (a.s.) ndiye mjuzi zaidi kuliko maswahaba wote   na ndiye anayefahamu sheria zaidi kuliko maswa-
haba wote, na kuwa laiti si Ali  (a.s.) basi wangeangamia, mpaka
ikafikia kauli ya Umar kuwa mfano halisi, nayo ni: “Laiti kama si Ali
Umar angeangamia.” Imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdullah
Al-Answar  kuwa  alisema: “Tulikuwa  hatuwatambui  wanafiki

isipokuwa kwa kumchukia Ali bin Abu Talib (a.s.).”

 

Zilipomfikia Muawiya habari za kuuwawa Ali (a.s.) alisema: “Sheria
na elimu yote imeondoka kwa kifo cha mwana wa Abu Talib.”

As-Shaabiy amesema: “Ali bin Abu Talib ndani ya umma huu ni sawa
na Masihi mwana wa Mariam kwa wana wa Israel: Kuna kundi
lililompenda mpaka likakufuru ndani ya mapenzi yake, na kundi
lingine likamchukia hivyo likakufuru kwa kumchukia.” Alikuwa
mkarimu sana. Alikuwa na maadili ayapendayo Mwenyezi Mungu
katika ukarimu, katu hakuwahi kumjibu mwombaji hapana sina.

Swaa’swaa’ bin Swawhan alimwambia Ali bin Abu Talib siku aliyopewa kiapo cha utii kuwa: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu ewe kiongozi wa waumini! Hakika umeupamba ukhalifa lakini wenyewe haujakupamba,  umeuinua  lakini  wenyewe  haujakuinua,  na  wenyewe unakuhitajia sana kuliko wewe unavyouhitajia.”

Ibnu Shabramat amesema: “Hakuna mtu yeyote asiyekuwa Ali bin Abu  Talib  mwenye  uwezo  wa  kusema  juu  ya  mimbari: ‘Niulizeni.’”

Qaaqaa bin Zararat alisimama kaburini kwa Imam Ali (a.s.) kisha akasema: “Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yako ewe kiongozi wa waumini, naapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hakika uhai wako ulikuwa ni ufunguo wa kheri, na laiti watu wangekukubali basi wangekula   toka juu yao na toka chini ya miguu yao, lakini wao wameidharau neema na wakaijali sana dunia.”

 

 

 

 

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani