Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Imam Ali(a.s)
Namba: 268145 Tarehe: 1390/00/00Rejea: ABNAprint

Historia ya Waja wema
Imam Ali(a.s)


 Imam Ali(a.s)

IMAM AMIRUL MUUMINIIN (A.S)

Yeye ni Ali bin Abi Twalib (a.s) na mama yake ni Fatuma binti Asad (a.s) nae ni mtoto wa Ami yake Mtume wa Allah (s.a.w) na mume wa binti yake na wasii wake na khalifa wake kwa watu baada yake, Amirul muuminiin na baba wa maimam (a.s).

Alizaliwa ndani ya Kaaba tukufu katika mji wa Makkah, siku ya ijuma tarehe kumi na tatu (13) ya mwezi wa Rajab baada ya miaka thalathini (30) tangu kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w) na alikufa shahidi usiku wa siku ya ijumaa katika msikiti wa Al-kufa katika mihrab, kwa upanga wa Ibnu Muljim Al-muradiy na bwana huyu alikuwa ni miongoni mwa Makhawariji– na ilikuwa ni tarehe kumi na tisa (19) ya mwezi mtukufu wa Ramadhan na kukutana au kurejea kwa mola wake baada ya siku tatu tangu apate dharuba lile na alikufa shahidi katika usiku wa tarehe (21) akiwa na umri wa miaka sitini na tatu (63), na maimam wawili Hassan na Hussen (a.s) ndio walio simamia suala la mazishi yake na kumzika katika mji wa Najaful-ashraf mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake hivi leo na kulificha kaburi lake kutokana na usia wake (a.s), ili liwe katika amani kutokana na mashambulizi ya makhawariji na wenye kulitembelea kaburi lake wasiweze kulifikia na kunufaika kwa kufanya hivyo  kisha imam Swadiq (a.s) akalitambulisha kwa watu pia imam Kaadhim (a.s).

Na anazo fadhila na sifa nyingi sana na zisizo hesabika, hakika yeye alikuwa ndie mtu wa kwanza kumuamini Mtume (s.a.w) na hakumshirikisha Mwenyezi Mungu hata chembe na wala hakusujudia sanamu kamwe na kutokana na hilo ndio maana ikasemwa kuwa linapo tajwa jina lake yasemwe maneno yafuatayo:Karrama llahu wajhahu (yaani Mwenyezi Mungu autukuze uso wake) na ushindi katika vita ulikuwa umefungamanishwa na bendera yake katika vita vyote, mwenye kusimama madhubuti na asie kimbia vitani, hakugeuka nyuma katika vita na wala hakukimbia kamwe na kutokana na hukumu zake nzuri ( au uzuri wa utoaji wa hukumu wa Ali Mtume akasema kuhusia nae: اقضاكم علي (Hakimu bora zaidi kati yenu ni Ali). Na kutokana na wingi wa elimu yake Mtume (s.a.w) akasema: أنا مد ينة العلم وعلي بابها (Mimi ni jiji la elimu na Ali ni mlango wake). na kutokana na kushikamana kwake na haki Mtume akasema: (علي مع الحق والحق مع علي) (Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali).

Na alikuwa ni muadilifu kwa watu wake, akitoa haki kwa sawa, mwenye kujiepusha na mali za kidunia, na alikuwa akija na kuingia kwenye hazina ya Waislaam (Baytul mali) na kuziangalia Dhahabu na Fedha na kusema:(يا صفراء ويا بيضاء غري غيري) (Ewe mwenye rangi ya manjano (Dhahabu) na ewe mwenye rangi nyeupe (Fedha) mghuri (mdanganye) mwingine tofauti na mimi). Kisha kuzitawanya kwa watu na habakishi hata tembe moja, na alikuwa akiwahurumia masikini na akikaa pamoja na mafukara na kukidhi haja za watu na akizungumza maneno ya haki na kweli na kuhukumu kwa uadilifu na kuhukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu.

Na alikuwa akitekeleza hukumu za Mwenyuezi Mungu, na akifuata mwenendo wa Mtume wa Allah (s.a.w) mpaka kheri ikaenea sehemu zote na baraka kutangaa na maisha bora na yenye neema (mazuri) kuwaenea waja wote na katika miji yote.

Kwa ufupi ni kuwa: Yeye (a.s) alikuwa kama Mtume (s.a.w) katika sifa zote na mambo yote, isipokuwa katika suala la Wahyi na Utume na kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu akamfanya katika aya ya maapizano (Mubahala) sawa na nafsi ya Mtume (s.a.w).
 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani