Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Imam Hasan(a.s)
Namba: 268987 Tarehe: 1390/00/00Rejea: Ripoti ya ABNAprint

Historia ya waja wema
Imam Hasan(a.s)


 Imam Hasan(a.s)

Yeye ni Haassan bin Ali (a.s) bin Abi Twalib, na mama yake ni Fatima Zahraa (a.s) binti Mohammad (s.a.w) nae ni mjukuu mkubwa wa Mtume (s.a.w) na ni khalifa wake wa pili na Imam wa watu baada ya baba yake Amirul muuminiin (a.s).

Amezaliwa katika mji wa Madinatul munawwarah siku ya juma nne katikati ya mwezi wa Ramadhan mwaka wa tatu wa hijiria, na alikufa shahidi kwa sumu ambayo alitegeshewa na Muawia bin Abi Sufyaan kupitia mkewe Imam Hassan ambae ni Juudah binti Ash'ath na hilo lilifanyika siku ya Al-khamisi tarehe saba (7) ya mwezi wa Safar  mwaka wa (50) hijiria, na alisimamia mazishi yake ndugu yake Imam Hussen (a.s) na kumsitiri katika makaburi ya Bakii’i katika mji wa Madinatul munawwarah, mahala ambapo ndipo kilipo kiwiliwili chake kwa hivi sasa (ndipo mahala lilipo kaburi lake) na-kwa masikitiko makubwa- kaburi lake lilivunjwa na Mawahabi pia walivunja kuba la kaburi lake hilo.

Na Imam Hassan (a.s) alikuwa ni mfanya ibada kwa wingi kati ya watu wa zama zake na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na mbora na alikuwa ni mwenye kumfanana sana Mtume (s.a.w), na alikuwa ni mkarimu zaidi kati ya Ahlul bayti wake katika zama zake na alikuwa ni mwenye huruma zaidi.

Na miongoni mwa ukarimu wake (a.s) ni kuwa alipewa mafuta uzuri na mjakazi mmoja wapo kati ya vijakazi wake, akasema kumwambia mjakazi yule: Wewe uko huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha akasema: Hivi ndivyo alivyo tuadabisha Mwenyezi Mungu pale alipo sema: واذا حييتم بتحية فحيوا بأحسن منها او رد واها) ) (Mnapo amkiwa kwa maamkizi basi itikieni kwa maamkizi mazuri zaidi kuliko mliyo amkiwa au rudisheni kwa yale maamkizi mliyo amkuliwa).

Na miongoni mwa upole wake (a.s) ni kuwa mtu mmoja wa Sham alimuona akiwa amepanda mnyama, yule bwana akawa akimlaani Imam na Imam hakumjibu kwa chochote, yule bwana alipo maliza kutoa laana zake na matusi yake Imam Hassan akamwendea na kusema: Ewe shekh nadhani ni mgeni na huenda umenifananisha, lau unge omba tukuridhishe basi tunge kuridhisha, na lau kama unge tuomba kitu fulani tunge kupatia na lau kama unge taka tukuongoze tunge kuongoza na lau unge tutaka tukubebee mzigo wako tunge kubebea na ikiwa unanjaa tunge kushibisha na kama unge kuwa uchi tunge kuvisha na kama ni muhitaji tutakutajirisha na ikiwa umefukuzwa tutakuhifadhi na kukusitiri na ikiwa unahaja tutaitatua haja yako.

Yule bwana alipo sikia maneno yale alilia na kusema: Nina shuhudia ya kuwa wewe ni Khalifa wa Mwenyezi Mungu katika Ardhi yake, hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kufahamu vema mahala pa kuuweka ujumbe wake.

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani