| Namba: 268988 | Tarehe: 1390/00/00 | Rejea: Ripoti ya ABNA | print |
Historia ya waja wema Imam Hussein(a.s) |
Yeye ni Hussen bin Ali bin Abi Twalib (a.s) na mama yake ni Fatima binti Mohammad (s.a.w) nae ni mjukuu wa Mtume (s.a.w) na Khalifa wake wa tatu na baba wa maimam tisa walio kuja baada yake na ni Imam wa watu baada ya nduguye au kaka yake Hassan (a.s).
Alizaliwa katika mji wa Madinatul-munawwarah tarehe tatu (3) ya mwezi wa Shaaban mwaka wa nne hijiria na kuuwawa kwa dhulma kwa upanga hali ya kuwa ni mwenye kiu, mauaji yaliyo fanya na bani Umayyah kwa amri ya Yazid bin Muawia katika tukio mashuhuri la Ashura, siku ya juma mosi tarehe kumi (10) ya mwezi wa Muharram mwaka (61) hijiria, na jeneza lake pia kiwiliwili chake kitwaharifu na kilicho katwa katwa kwa mapanga pamoja na viwiliwili vingine vya mashahidi walio kufa mashahid pamoja nae vilizikwa baada ya siku tatu tangu kuuwawa kwao wakiwa mashahidi na alaie mzika ni mwanae Imam Zainul aabidiin (a.s) na kumzika mahala ambapo ndipo kaburi lake lilipo hivi sasa katika mji mtukufu wa Karbalaa, mji ambao uliangukia mikononi mwa Saddam na kundi lake na Mwenyezi Mungu kuukomboa kutoka mikononi mwao-pamoja na sehemu zingine tukufu zilizoko Iraq.
Na fadhila zake ni nyingi sana kiasi kwamba ni vigumu kuweza kuzitaja zote, kwani yeye ni ua zuri la Mtume (s.a.w) ambae Mtume alisema kuhusiana na yeye: حسين مني وانا من حسين Hussein anatokana na mimi na mimi natokana na Hussen.[15]
Na pia amesema kuhusiana nae na kuhusu nduguye Hassan (a.s):
هم ريحانتياي من الد نيا
(Wao wawili ni maua yangu mazuri duniani).[16]
Pia amesema (s.a.w):الحسن والحسين سيدا شباب اهل الجنة
Hassan na Hussedin ni mabwana wa vijana wa peponi.[17]
Pia amesema (s.a.w):
الحسن والحسين إمامان قاما أو قعدا [18]
Hassan na Hussein ni maimam sawa wakiwa wamesimam au wamekaa.
Na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na mfanya ibada sana kati ya watu, hakika alikuwa akisali kila usiku rakaa elfu moja kama baba yake Amirul muuminiin (a.s) na mara nyingi alikuwa akibeba mfuko wa ngozi wenye vyakula usiku na kuwapelekea mafakiri hadi ilionekana alama na athari yake mgongoni mwake baada ya kuuliwa na alikuwa ni mkarimu, mtukufu, mpole, na alikuwa mkali sana pindi anapo asiwa Mwenyezi Mungu.
Na miongoni mwa ukarimu wake ni pale alipojiwa na bedui mmoja akimuomba na kumuimbia shairi lisemalo: Hakwenda kombo kwa hivi sasa mwenye kukuelekea kwa matarajio na alie bisha mlangoni kwa mara kadhaa, wewe ni mkarimu na wewe ni mwenye kutegemewa, baba yako alikuwa ni muuaji wa mafasiki, lau kama si yule ambae alikuwa mwanzoni mwenu, basi sisi sote tunge enewa na kuzungukwa na moto wa jahannama.
Imam Hussen akampatia dinari elfu nne na akmuomba msamaha kwa kusema: Zichukue hakika mimi nakuomba samahani na fahamu ya kuwa mimi ni mwenye huruma sana kwako, lau kama mwendo wetu kesho ungekuwa ni mwema, na anga letu lingekumiminia kheri nyingi, lakini matatizo ya zama ni ya aina tofauti na yenye kubadilika kwa hivyo na mkono wangu ni wenye kutoa kidogo.
Na kwa hakika Imam (a.s) kwa kisimamo chake cha kishujaa-na ambacho hakina mfano katika ulimwengu-aliweza kuihuisha sheria ya kiislaam na dini ya babu yake Mtume (s.a.w) bali aliuhuisha ulimwengu wote hadi siku ya kiama, kwa hivyo yeye ni bwana wa mashahidi na ni mtu bora baada ya kaka yake na nduguye Hassan (a.s).