| Namba: 268991 | Tarehe: 1390/00/00 | Rejea: Ripoti ya ABNA | print |
Historia ya waja wema Imam Baqir(a.s) |
Yeye ni Imam Mohammad bin Ali Al-baaqir (a.s) na mama yake ni Fatuma binti Hassan (a.s) alizaliwa katika mji wa madina siku ya Ijumaa mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Rajab mwaka (57) hijiria. Na yeye ndie mtu wa kwanza katika kizazi cha Ali alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi hicho cha Ali, na ni mtu wa kwanza wa kizazi cha Haashim alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi cha Haashim, na ni mtu wa kwanza alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi cha Fatuma, kwani yeye ndie wa mwanzo alie kusanya kati ya kizazi cha maimamu wawili Hassana na Hussen (a.s) na alikufa shahidi kwa sumu siku ya juma tatu tarehe (7) Dhul hajjil haraam mwaka (114) hijiria akiwa na umri wa miaka (57) na mwanae Imam Swaadiq (a.s) ndie alie simamia suala la maandalizi ya mazishi yake na kumzika pembezoni mwa kaburi la baba yake Imam Sajjad (a.s) na Ami wa baba yake na babu yake Imam Mujtaba (a.s) katika makaburi ya Baqii'i kwenye mji wa Madinatuil munawwarah.
Na alikuwa ni mwenye fadhila kubwa mkarimu na mwenye kushikamana na dini na alikuwa ni mwenye elimu nyingi na kubwa na mpole sana, pia mwenye tabia njema na mwenye kufanya ibada sana, mwenye unyenyekevu, ukarimu, ukunjufu na alifikia kwenye kilele katika tabia zake njema, mkiristo mmoja alimwambia: Wewe ni mfunguzi na mpasuaji!
Imam akasema: Mimi ni Mfuinguzi.
Akasema wewe ni mtoto wa mpishi.
Imam akasema: Hiyo ni kazi yake.
Akasema: Wewe ni mtoto wa mtu mweusi na mbaya.
Imam (a.s) akasema: Ikiwa umesema kweli Mwenyezi Mungu amsamehe na ikiwa umesema uongo Mwenyezi Mungu akusamehe.
Yule Mkiristo akasilimu.
Na katika elimu alikuwa kama Bahari yenye mawimbi mengi, akijibu kila mas'ala na swali lolote analo ulizwa bila kusita. Na Ibnu Atwaa Al-makiy amesema: Sija wahi kuona kamwe wanazuoni na maulamaa kwa mtu yeyote alie kuwa mdogo zaidi kuliko nilivyo waona kwa Baaqir (a.s) hakika nilimuona Al-hakam bin Utaybah-pamoja na utukufu wake na heshima yake kati ya watu-akiwa mbele yake kama mtoto akiwa mbele ya mwalimu wake, na Mohammad bin Muslim amesema: Sikujiwa na fikra yoyote isipokuwa nilimuuliza Mohammad bin Ali (a.s) mpaka nilimuuliza hadithi elifu thalathini (30).
Na Imam (a.s) alikuwa ni mwenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wakati wote, mpaka Imam Swaadiq (a.s) akasema: Baba yangu alikuwa ni mwenye kumtaja sana Mwenyezi Mungu, nilikuwa nikitembea pamoja nae hali ya kuwa akimtaja Mwenyezi Mungu na alikuwa akizungumza na watu na lisimshughulishe hilo kunako kumtaja Mwenyezi Mungu.
Na Imam alikuwa ni mwingi wa tahajjud (sala za usiku) na ibada, mwenye kulia sana na mwenye mazingatio.