| Namba: 268992 | Tarehe: 1390/00/00 | Rejea: Ripoti ya ABNA | print |
Historia ya waja wema Imam Ja'afar Sadiq(a.s) |
Yeye ni Jaafar bin Mohammad As-swaadiq (a.s) na mama yake ni Fatuma alie kuwa akiitwa kwa kunia ya (Ummu farwah) alizaliwa (a.s) katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarehe (17) mwezi wa Rabiiul Aawwal (mfungo sita) siku ya kuzaliwa Mtume (s.a.w) mwaka (83) hijiria na kufa shahidi kwa sumu siku ya juma nne tarehe (25) mwezi wa Shawwal (mfungo mosi) mwaka (148) hijiria akiwa na umri wa miaka (65), na mwanae Imam Kaadhim kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika katika makaburi ya Baqii'i pembezoni mwa kaburi la baba yake Imam Baaqir (a.s) na babu zake wawili: Imam Sajjad na Imam Mujtaba (a.s).
Na alikuwa na Fadhila nyingi zisizo hesabika kama elimu, fadhila, hekima, fiqhi, zuhdi, uchamungu, ukweli, uadilifu, ubora, furaha na utoaji, ukarimu, ushujaa na fadhila zinginezo.
Na kwa hakika Mufiid alisema (Mwenyezi mungu autukuze utajo wake): Na maulamaa hawakunukuu kwa yeyote kati ya Ahlul bayti wake kama walivyo nukuu kutoka kwake na hakuna yeyote kati ya watu wakusanyao hadithi na wakusanyaji wa habari, mfano wa Jaafar bin Mohammad As-swaadiq (a.s) hakika walikusanya majina ya wapokezi kutoka kwake kati ya watu waaminifu pamoja na kutofautiana kwao kirai na itikadi, na walikuwa ni watu elfu nne (4000) [25] …. Hadi mwisho wa maneno yake.
Na Abu hanifa Imamu wa madhehebu ya hanafi alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wake moja kwa moja, kama ambavyo maimam wengine wa madhehebu za Ahli sunna walikuwa ni wa wanafunzi wake pia (a.s) lakini si moja kwa moja bali kwa kupitia wanafunzi wake na kwamba elimu nyingi na mpya kama vile Kemia, Fizikia na elimu ya maumbo na nyota na elimu ya ugunduzi wa madini na kuchimbuaji wa hazina zilizoko ardhini na zinginezo nyingi ambazo Imam ndie alie weka misingi yake na kuwaongoza watu kwenye elimu hizo.
Hakika Imam (a.s) alitumia fursa iliyopatikana ya ugomvi kati ya bani Abbas walio fanya mapinduzi dhidi ya bani Umayyah na kati ya bani umayya walio kuwa mbioni kuanguka na kutoweka dola lao, alitumia fursa hiyo kuanzisha Madrasa kubwa ya kielimu na kujishughulisha na kazi ya ulezi wa wanafunzi na watafutaji wa elimu na kuwabainishia mafunzo ya kiislaam na uzuri wa sheria zake na kuwafafanulia fikra za batili na mbaya zilizo ingia kwenye Uislaam na kubatilisha shubha zitolewazo, mpaka misingi ya sheria ikaimarika na ubainifu wa Uislaam kudhihiri na kubainika wazi na akafahamika (a.s) kama Raisi na kiongozi wa Madhehebu ya Jaafaria, kama ambavyo wafuasi wake (a.s) walifahamika pia kwa jina la Shiatu Jaafar (wafuasi wa Jaafar au mashia wa Jaafar).
Na miongoni mwa uongofu wake (a.s) ni kuwa yeye alikuwa akila siki na mafuta na kuvaa kanzu ngumu na nzito napengine alikuwa akivaa nguo yenye viraka na alikuwa akifanya kazi zake mwenyewe kwenmye mabustani na mashamba yake.
Na miongoni mwa Ibada zake ni kuwa alikuwa akisali sana na pengine alikuwa akizimia katika sala na kuitwa watu wa kumsaidia usiku, Mtumishi wake anasema: Nilikwenda mlangoni kwake na nikamkuta katika chumba chake cha faragha akiwa ameweka shavu lake juu ya udongo hali akiomba kwa kuinua vitanga vyake na huku kukiwa na athari ya mchanga usoni mwake na kwenye shavu lake.
Na Imam (a.s) alikuwa ni mwingi wa kutoa, mwenye tabia njema, mwenye maneno laini, mwenye vikao vizuri na mwenye bashasha kwa kila mwenye kukutana nae na alikuwa na muashara mzuri kwa kila anae kutana nae.