Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Imam Ridhaa(a.s)
Namba: 268994 Tarehe: 1390/00/00Rejea: print

Historia ya waja wema
Imam Ridhaa(a.s)


 Imam Ridhaa(a.s)

Yeye ni Imam Ali bin Mussa Ridhaa (a.s) na mama yake ni Sayyidah Najmah, alizaliwa (a.s) siku ya Al-khamisi tarehe (11) mwezi wa Dhulqaadatul-haraam, mwaka (148) hijiria katika mji wa Madina na kufa shahidi kwa sumu siku ya Ijumaa mwishoni mwa mwezi wa Safar, mwaka (203) na mwanae Imam Jawaad (a.s) kusimamia suala la maandalizi ya mazishi yake na kumzika katika sehemu ya khorasani sehemu ambayo ndiko liliko kaburi lake tukufu.

Na Imam (a.s) alikuwa mashuhuri sana kwa elimu nyingi, fadhila, ukarimu, mwingi wa kutoa, mwenye tabia njema, mnyenyekevu, na mwenye kufanya ibada sana.

Maamun-kutokana na vitimbi na hadaa-alimuita Imam Ridhaa (a.s) kutoka Madinah hadi Khorasani (Iran) na kumtaka achukue ukhalifa wa kiislaam-badala yake-lakini Imam alikuwa amejiweka kando na kuyapa mgongo mambo ya kidunia (yaani alikuwa ni mwenye zuhdi) na hakukubali, kwani alifahamu matokeo ya maombi hayo, kuwa ni vitimbi na hadaa, kama ambavyo babu yake Amirul muuminiin (a.s) alivyo kataa Ukhalifa-katika shura-wakati Ibnu Auf alipo mpatia Ukhalifa huo kwa sharti kwamba afuate sera ya mashekhe wawili walio mtangulia, (Abubakar na Omar), kwani Imam aliona ya kuwa Ukhalifa wakati huo ulikuwa umesimama juu ya jambo moja wapo kati ya mambo mawili, na mambo yote mawili hayo ni ya uongo na si yenye kukubaliwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu: Ama jambo la kwanza ni kuwa Imam (a.s) akubali sharti kisha asilitekeleze-kama alivyo fanya Othumani-na huo ni uongo wa kikauli na wenye kuchukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Ama jambo la pili ni kuwa: Imam akubali sharti na atekeleze, maana yake ni kuwa aridhie sera ya mashekhe wawili pamoja na kuwa hakuwa na ridhaa na hakuridhishwa na matendo yao na huo ni uongo wa kimatendo na ni wenye kukemewa mbele ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo basi Imam hakuona njia yenye kuridhiwa na Mwenyezi Mungu tofauti na kukataa na kupinga na kuto kubali.

Na baada ya Imam Ridhaa (a.s) kuukataa Ukhalifa, Maamun alishikwa na butwaa na kunyongea sana kwani aliona ya kuwa mpango wake ambao kwa ajili yake alimuita Imam umeshindwa na kufeli, hapo alimtaka achukue wilayatul ahad -cheo cha waziri mkuu- na kumlazimisha kukubali (a.s) lakini Imam (a.s) alimuwekea sharti ya kuwa hato ingilia katika jambo lolote kati ya mambo ya dola na kukubali cheo hicho kwa sharti hilo.

Imam (a.s) alikuwa ni mrithi wa baba zake watukufu (a.s) katika elimu na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) na elimu yake ilionekana na kudhihiri kiasi kidogo kuhusiana na mambo ya dini na Madhehebu fikra na Itikadi-katika kikao cha majadiliano ambacho kiliandaliwa na Maamuun-na yaliyo jitokeza kwenye hadithi ya Rukbaan.

Vile vile katika ibada alikuwa (a.s) akikesha katika masiku mengi kwa ibada na kuhitimisha Qur'ani kwa muda wa siku tatu na mara nyingi alikuwa akisali usiku na mchana rakaa elfu moja, na mara nyingi alikuwa akisujudu kwa muda mrefu, pengine alichukua masaa kadhaa kwenye sijda na alikuwa ni mwengi wa kufunga.

Na Imam (a.s) alikuwa ni mwingi wa kutenda mema, na akitoa sana sadaka na sadaka nyingi alikuwa kizitoa kwa siri na hasa kwenye usiku wa kiza.

Na miongoni mwa tabia zake na adabu zake (a.s) ni kuwa hakumuudhi mtu yeyote kwa maneno kamwe na wala hakumfanyia ukali mtu yeyote katika kauli, na hakuwa akiegemea kukiwa kuna watu wamekaa mbele yake na hakuwahi kucheka kwa sauti kubwa na ya juu kamwe, na hakuwahi kutema mate mbele ya yeyote kamwe, na chakula kilipo kuwa tayari mezani huwaita ahli zake wote na wahudumu wake na kula pamoja nao.
 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani