| Namba: 268995 | Tarehe: 1390/00/00 | Rejea: Ripoti ya ABNA | print |
Historia ya waja wema Imam Jawad(a.s) |
Yeye ni Imam Mohammad bin Ali Al-jawaad (a.s) na mama yake ni Sayyidah Sabiika, alizaliwa (a.s) siku ya Ijumaa tarehe (10) katika mwezi mtukufu wa Rajab, mwaka (195) hijiria, katika mji wa Madinatul munawwarah na kufa shahidi kwa sumu katika mji wa Baghdaad, mwishoni mwa mwezi wa Dhul-qaadah (mfungo pili) mwaka (220) hijiria, na mwanae Imam Al-hadiy (a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika kwenye maburi ya Makuraishi pembezoni mwa kaburi la babu yake Muusa bin Jaafar (a.s) katika mji wa Kaadhimiyyah mahala lilipo kaburi lake kwa hivi sasa.
Na Imam (a.s) alikuwa ni mjuzi zaidi kati ya watu wa zama zake na mbora zaidi kuliko watu wote, mkarimu, pia mwingi wa kutoa na mwenye vikao vizuri, na alikuwa ni mwenye tabia njema, mfasaha na kila alipo kuwa akipanda mnyama wake hubeba Dhahabu na Fedha na hakuna aliekuwa akimuomba isipokuwa humpatia, na alie kuwa akimuomba pamoja na wingi wao alikuwa hampatiii chini ya Dinari Khamsini (50) na alie kuwa akimuomba kati ya shangazi zake alikuwa hampi chini ya Dinari ishirini na tano (25).
Na miongoni mwa elimu yake kubwa ambayo ilidhihiri kwa watu: Ni kuwa wanazuoni thamanini kati ya wanazuoni wa miji mbalimbali walikusanyika kwake baada ya kurudi kwao kutoka kwenye ibada ya hijja na kumuuliza kuhusiana na mas'ala mbali mbali na yeye (a.s) kuwajibu, namiongoni mwa mambo ya ajabu yaliyo simuliwa kutoka kwake (a.s) ni kuwa watu wengi walikusanyika kwake na kumuuliza mas'ala thelethini elfu-katika kikao kimoja nacho ni kikao kiitwacho kwa siku hizi kwa jina la kongamamno, kongamano ambalo hufanyika na kuendelea kwa muda wa siku kadhaa na Imam kuwajibu mas'ala hayo bila kusita kufanya hivyo wala kukosea na wakati huo akiwa na umri wa miaka tisa (9), lakini jambo kama hili si jambo la ajabu na la kushangaza kutokea kwa Ahlul bayti-watu wa nyumba ya Wahyi na mahala alipokuwa Jibril (a.s) akitelemka akiwa na Qur'ani na hasa baada ya Qur'ani kuzungumzia kuhusiana na kupewa kwa Issa bin Maryam kitabu na Utume hali ya kuwa bado yuko kwenye kitanda chake akiwa mtoto mchanga.
Kisha ni kuwa khalifa Alimuoza binti yake na hilo lilifanyika baada ya kumtahini kwa maswali (mas'ala) muhimu na kuyajibu yote-katika kisa mashuhuri.