| Namba: 268996 | Tarehe: 1390/00/00 | Rejea: Ripoti ya ABNA | print |
Historia ya waja wema Imam Al-haadi |
Yeye ni Imam Ali bin Mohammad Al-hadiy (a.s) mama yake ni Sayyidah Samanah.
Alizaliwa (a.s) katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarehe (2) mwezi mtukufu wa Rajab, mwaka (212) hijiria na kufa shahidi kwa sumu kwenye mji wa Samarraa siku ya juma tatu tarehe (3) mwezi wa Rajab, mwaka (254) hijiria, na mwanae Imam Askariy (a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake, na kumzika ndani ya nyumba yake kwenye mji wa Samarraa mahala lilipo kaburi lake kwa hivi sasa na mahala kilipo lazwa kiwili wili chake kitukufu.
Na Imam (a.s) alikuwa ni mtu bora kati ya watu wa zama zake na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na alie kusanya fadhila zote na mkarimu sana na mwingi wa kutoa na alikuwa ni mwenye maneno laini na aliekuwa akimuabudu sana Mwenyezi Mungu na mwenye sera nzuri nasafi na mwenye tabia njema.
Na miongoni mwa ukarimu wake ni kisa kilicho pokelewa na (Ardabiliy) katika kisa chake ya kuwa: Khalifa alimtumia Dirham elfu thalathini, Imam akampatia bedui mmoja wa Al-kufa kama zawadi na akamwambia: Toa kiasi ulipe madeni yako na kiasi kitakacho bakia kitumie kwa ajili ya matumizi na mahitaji ya familia yako na ahali zako na utusamehe.
Yule bedui akamwambia Imam: Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika deni nililo kuwa nalo halifikii theluthi ya pesa hii. (Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kufahamu vema mahala pakuuweka ujumbe wake), na akachukua pesa zile na kwenda zake.