Abna inaendelea kutuarifu kuwa:Brigedia
Salami amesema kuwa, madai hayo ya Marekani yasiyokuwa na mashiko wala
msingi ni moja kati ya njama za dola hilo la kibeberu za kujaribu
kuichanganya jamii ya kimataifa mkabala na kuelekea kufeli kwa mfumo
wake wa kibepari. Matamshi ya afisa huyo wa ngazi za juu wa jeshi la
Iran yanaenda sambamba na tamko la Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
aliyesema kuwa, tuhuma hizo za Marekani ni mchezo uliofeli na hata
Wasaudia wenyewe wanaelewa vyema mchezo huo na taathira zake. Waziri wa
Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa uhusiano wa Iran na nchi za Ghuba
ya Uajemi ni mzuri.Serikali Tehran imesisitiza kwamba, uhusiano wake na Serikali ya Riyadh ni mzuri licha ya hitilafu za kimtazamo ziliopo kati ya pande hizo
mbili kuhusu matukio ya eneo la Mashariki ya Kati.